• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Vifaa vya Milioni 9 vya maabara vyakabidhiwa Dodoma

Imewekwa tarehe: September 18th, 2023

Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KUSINI

ELIMU ndiyo mkombozi kwa vijana wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuwasaidia kutoa mchango katika maisha yao na maendeleo ya taifa la Tanzania.

Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde alipokuwa akiongea na wanafunzi na walimu wa shule za sekondari katika hafla ya kugawa vifaa vya maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi tukio lililofanyika Shule ya Sekondari Wella iliyopo Kata ya Kikuyu Kusini.

Mavunde ambae pia ni Waziri wa Madini alisema “elimu ninaamini kwamba ndiyo mkombozi wa kweli kwa vijana wetu na elimu hii itawasaidia kwenda kuwafanya wakatoe mchango wao na kulitumikia taifa la Tanzania na wao pia katika maisha yao. Baada ya kubaini tunachangamoto katika maabara zetu nyingi za vifaa, nikasema nianze na awamu ya kwanza na hii haitakuwa mwisho nitajitahidi kuzifikia maabara nyingi zaidi. Leo nimeanza na shule tatu na mzigo wa kwanza huu umenigharimu shilingi 9,000,000 na nitaendelea kufanya hivi sababu dhamira yangu ni kuhakikisha wanafunzi wetu wanafanya vizuri”.

Akielezea mikakati yake kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema ni kukuza elimu. “Mkakati wa kwanza ambao ninao kwenye kukuza elimu katika Mkoa wa Dodoma na hasa Jimbo la Dodoma mjini. Nimesikia changamoto ya walimu wa sayansi hii ni changamoto kubwa na mimi suluhisho ninalo na nimeshaanza kulifanyia kazi. Tuna shule za sekondari 43, lakini Dodoma umepita Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao una uwezo wa kutuunganisha kupitia teknolojia ya kisasa mwalimu mmoja wa sayansi mfano wa Shule ya Sekondari Msalato anaweza akawafundisha wanafunzi wote wa Dodoma kwa wakati huohuo. Tukipata seti 43 za televisheni zikafungwa shule zote, mimi kwa nafasi yangu nitakwenda kuongea na TCRA na watu wa Mfuko wa Mawasiliano na kampuni za simu niwaombe watuunganishie huu mkongo” alisema Mavunde.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alisema kuwa halmashauri yake imepeleka shilingi 20,000,000 kukamilisha ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari Wella. “Mheshimiwa mbunge, hapa tayari unaona ujenzi unaendelea kwenye maabara yetu kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais, sisi hatuwezi kukuangusha kwa sababu tunafanya kazi kwa kushirikiana tumeshaleta shilingi 20,000,000 hapa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara. Mheshimiwa waziri kwa maelekezo yako ya juzi ulituelekeza tutafute fedha na tumeshapata shilingi 8,000,000 kwa ajili ya kukamilisha matundu saba ya vyoo. Miongoni mwa changamoto ambazo zimezungumzwa na mkuu wa shule nimezipokea na nitakaa na timu yangu ya menejimenti na madiwani tuone namna bora ya kuzitatua” alisema Kayombo.

Aidha, alishukuru kwa vifaa vya maabara vilivyokabidhiwa na mbunge. “Mheshimiwa waziri, vifaa hivi ulivyotukabidhi leo ninakushukuru sana, ni miongoni mwa wabunge wachache wanaoyapenda majimbo yao. Mimi hii ni halmashauri yangu ya nne kama mkurugenzi, lakini nimekuwa nikikufuatilia sana kote nilipokuwa unapambana sana kuhakikisha jimbo lako linaenda vizuri, siyo kwenye elimu tu bali kwenye maeneo yote. Nikuombe moyo huu uendelee na sisi tupo bega kwa bega na wewe tutakupa ushirikiano wa kutosha na hakuna atakayekuangusha” alisema Kayombo.

Awali akiongelea mafanikio ya shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Wella, Mwl. Adelifi Kaizirege alisema kuwa shule yake imefanikiwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi mwaka hadi mwaka. “Sambamba na hilo shule imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga kidato cha tano na vyuo vya kati. Kufanya ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa kwa kuweka sakafu chini kupitia michango ya wazazi na wadau wa shule na kuongeza vyumba vitatu vya madarasa” alisema Kaizirege.

Kuhusu malezi na nidhamu ya wanafunzi alisema kuwa imeimarika sana. “Nidhamu ya wanafunzi imeimarika kutokana na juhudi ambazo uongozi wa shule kwa kushirikiana na walimu unazitumia na kuzisimamia. Wanafunzi wengi wanajitahidi kuwahi kufika shuleni kutokana na usimamizi wa walimu. Uongozi wa shule unawapongeza wazazi wote wanaotoa ushirikiano chanya katika kutatua changamoto za kinidhamu zinazowakabili watoto wao hasa utoro, kunyoa mitindo, kutoboa pua, kuvaa sketi fupi, kuvaa suruali zinazobana, kujihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi na ugomvi” alisema Kaizirege.

Jumla ya shule tatu za sekondari Wella, Makutopora na Mtemi Chiloloma zilipokea vifaa vya maabara za masomo ya sanyansi vyenye thamani ya shilingi 9,000,000.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde alipokuwa akiongea na wanafunzi na walimu wa shule za sekondari katika hafla ya kugawa vifaa vya maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi tukio lililofanyika Shule ya Sekondari Wella iliyopo Kata ya Kikuyu Kusini.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo akiongea katika makabidhiano hayo ambapo amempongeza Mbunge Mhe. Mavunde na kuahidi kuendelea kuchangia kwenye miradi ya maendeleo itakayosaidia kuinua elimu jijini Dodoma.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wella waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya vifaa vya maabara za sayansi.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.